Wizara Ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida

SUWASA YASHIRIKI KATIKA KIKAO CHA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA SINGIDA MJINI.


Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) imeshiriki katika kikao cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya katika kupitia taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha mapinduzi (CCM) 2020-2025 kuanzia mwezi Januari mpaka Desemba, 2025.
Kikao hicho kimefanyika tarehe 10.03.2026 katika ukumbi wa Veta Singida kimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wilaya na Mkoa wakiwemo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Katibu Mwenezi Wilaya na Mkoa, Mwenyekiti na Katibu CCM Wilaya,Madiwani, Watendaji wa kata, Wenyeviti wa Mitaa, Viongozi wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama pamoja na Viongozi wa Mashirika mbalimbali ya Wilaya.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya Mh. Lucia Mwiru amefungua kikao hicho kwa kupongeza zoezi zima la uchaguzi Mkuu wa uliofanyika mwezi Octoba.29.2025 nchini kwa kuwa wa amani na utulivu hasa katika mkoa wa Singida hali iliyopelekea viongozi mbalimbali kuweza kupatikana na kura nyingi kwa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pia amewasisitiza wananchi waendelee kuwa wamoja na kudumisha amani ili utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo iweze kutekelezwa kama ambavyo ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inavyoelekeza.
Kwa upande wa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Singida Mjini Mh Thomas Apson ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi akiwasilisha taarifa hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Singida Mh Godwin Gondwe amepongeza mwenendo mzuri wa utekelezaji wa miradi mbali mbali ya kimaendeleo katika Sekta zote muhimu kama Maji, Afya, Barabara na Umeme amesisitiza kila mmoja aendelee kuweka jitihada na taaluma ili kuhakikisha ilani ya Chama inatekelezwa kikamilifu ili kuondoa na kumaliza kero zinazowakabili Wananchi.
Kwa upande wa sekta ya maji Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na usafi wa Mazingira Singida ndg Hosea maghimbi akiwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama ameeleza katika utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi Suwasa imeendelea kuboresha huduma ya maji safi kwa wananchi ambapo kwa sasa upatikanaji wa maji safi umeongezeka ambao ni asilimia 77 .
Aidha ameeleza kuwa Mamlaka imekamilisha ujenzi wa bwawa la kutibu maji la Manga wenye thamani ya TZS 1,348,761,617.59, Pia ukarabati na kupanua mtandao wa maji katika Manispaa ya Singida yenye thamani ya TZS 424,442,117.81 pamoja na Uchimbaji wa kisima katika chanzo cha maji Mwankoko wenye thamani ya TZS 92,004,010.
Katika Kikao hicho kilichoongozwa na Mh Lucia Mwiru Mwenyekiti wa CCM Wilaya alitoa nafasi ya Wajumbe mbalimbali kuchangia hoja mbalimbali na kuuliza maswali juu ya Taarifa iliyowasilishwa na kuhakikisha maswali na mapendekezo hayo yafanyiwa kazi na majibu kupatikana.
Hoja zote za wajumbe zinazohusu masuala ya maji zilizowasilishwa na wajumbe zimeweza kujibiwa .
Aidha taarifa hiyo ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha mapinduzi imejadiliwa kwa kina na kupitishwa na wajumbe wote.
Mwenyekiti amesisitiza jitihada ziendelee kwa kila mmoja wa Chama na Serikali katika utendaji wa kazi na kusimamia nyanja zote muhimu ili kumsaidia Mh. Rais katika kuwatumikia wananchi na kutatua kero zote zinazowakabili ili kujenga imani na Serikali yao.
## Kazinautu tunasongambele