MRADI WA UBORESHAJI WA HUDUMA YA MAJI SAFI MTIPA WATEMBELEWA KATIKA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI ITAKAYOKAGULIWA NA MWENGE WA UHURU 2026 MKOA WA SINGIDA KATIKA - HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA
Jana Tarehe 21 Mei 2026, Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Singida, amefanya ziara kwaajili ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo inayotarajiwa kuzinduliwa, kuwekwa jiwe la msingi pamoja na kutembelewa na Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2026 katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida.
Ziara hiyo imelenga kuhakikisha miradi yote inayopitiwa na Mwenge wa Uhuru imekidhi viwango vyote vya ubora pamoja na kuendana na thamani halisi ya fedha za Serikali katika kuwahudumia wananchi.
Katika ziara hiyo Mradi wa SUWASA ambao umekaguliwa ni Mradi wa Uboreshaji wa Huduma ya MajiSafi uliopo kata ya Mtipa katika eneo la Mtipa Mashariki.
Katika ziara hiyo, Mhe. Dendego alisisitiza umuhimu wa kuzingatia usafi wa mazingira katika maeneo ya miradi na kuhakikisha ubora wa utekelezaji wa mradi.
Aidha, alieleza kuwa Mwenge wa Uhuru unaendelea kuwa chombo muhimu cha kuhamasisha maendeleo, uwajibikaji na ushirikishwaji wa wananchi katika miradi yenye tija kwa jamii.
#Kazinautu tunasongambele #