Wizara Ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida

WATUMISHI WA SUWASA WASHIRIKI MAFUNZO YA MFUMO WA UTENDAJI KAZI KIDIJITALI WA e-OFFICE (OFISI YA KIELETRONIKI)


Watumishi wa Mamlaka ya majisafi na Usafi wa Mazingira Singida Siku ya jana tarehe 08.06.2026 wameshiriki katika mafunzo ya mfumo wa utendaji wa kazi kidijitali uitwao e-office yaani Ofisi ya Kieletroniki yaliyofanyika katika Ofisi za Suwasa zilizopo Utemini.


Mafunzo hayo yameendeshwa na Mkufunzi aitwaye

Ally Athumani Ally ambaye ni Afisa Tehama wa Wakala wa Serikali Mtandao yaani "eGA" Makao makuu Dodoma.


Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo watumishi katika kufanya kazi kidijitali kupitia mfumo huo ili kuboresha utendaji, kuokoa muda na kupunguza matumizi ya karatasi kwani kazi nyingi za kawaida zinafanywa kwa kutumia kompyuta, simu na   mtandao 


Aidha ameeleza kuwa kazi kubwa ya Ofisi ya Kielektroniki  ni pamoja na 

Kubadilisha kazi za karatasi  kuwa digital. ili kufanya kazi iwe haraka, isiyo na ufisadi na inayofuatiliwa. Pia inaongeza uwazi na kupunguza gharama kwani mtumishi anaweza kufanya kazi akiwa mahala popote.


Aidha ameitaka Suwasa kuanza kutumia mfumo huo ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi wa Singida. 


##kazinaututunasongambele.