ALIYEKUWA MKURUGENZI MTENDAJI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA AFANYA MAKABIDHIANO YA OFISI NA MKURUGENZI MPYA WA SUWASA MHA. RAMADHANI MTINDASI
Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) Bw. Sebastian V. Warioba akiwa na Mkurugenzi Mpya Mhandisi Ramadhani Mtindasi na Menejimenti ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira wamefanya kikao cha makabidhiano ya Ofisi leo tarehe 11.06.2026 mara baada ya kuteuliwa kituo kipya cha kazi na Mh. Waziri wa Maji Jumaa Awesso kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira Sengerema(Seuwasa)
Bw. Sebastian V. Warioba pamoja na Management yote ya Suwasa wamemkaribisha Mkurugenzi Mpya Mha. Ramadhani Mtindasi katika Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) na kumsihi aendelee kufanya kazi Kwa bidii ili kufikia Malengo ya SUWASA Kwa Wateja wa Singida kwani Singida wanahitaji sana Huduma yake.
Pia wamemtakia kila la Kheri katika Majukumu yake Mapya ya Kazi na kuishi vyema na Watumishi.
Aidha Mkurugenzi mpya Mh. Ramadhani Mtindasi amepokea Vema ukaribisho huo na Kumshukuru Bwa
Sebastian V.Warioba Kwa kumkaribisha vema SUWASA na kumuahidi kuwa atafanya kazi Kwa bidii ili kufikia Malengo ya WanaSingida na kuhakikisha huduma ya Majisafi na usafi wa Mazingira inakuwa endelevu.
Pia ameiomba Menejimenti ya SUWASA kuwa na ushirikiano katika Kutekeleza Majukumu yake Mapya ya Kazi kwani yeye amekuja kufanya kazi na Watu Kwa Upendo na Kwa Ushirikiano.
Nae Kaimu Mkurugenzi wa Huduma Kwa Wateja Ndg Hosea JP. Maghimbi amemshukuru Bw. Sebastian V. Warioba Kwa Uongozi wake mwema katika wakati wote alioutumia Kwa kufanya kazi Kwa weledi na uzalendo mkubwa akiwa SUWASA.
Pia kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Bi. Sara Maira amemkaribisha Mkurugenzi Mpya Mha. Ramadhani Mtindasi na kumuahidi kuwa watampa Ushirikiano wa Hali ya juu katika Majukumu yake ya Kazi ili kufikia Malengo ya WanaSingida Kwa pamoja.
Aidha wote kwa pamoja wamemtakia Majukumu mema Bw. Sebastian V. Warioba katika kituo chake kipya cha kazi.
###kazinaututunasongambele.