Wizara Ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida

SUWASA YASAINI MKATABA WA UJENZI NA KAMPUNI YA HOKKAIDO INTERNATIONAL CONTRACTORS COMPANY LIMITED


Mamlaka ya Maji Safi na Usafi waMazingiraSingida (SUWASA) leo tarehe 13.03.2026 imesaini mkataba wa Ujenzi na Kampuni ya Hokkaido international Contractors Company Limited

Ujenzi huo unahusisha Tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa 100m³, ujenzi wa Ofisi, Kituo cha kuchotea Maji majumbani, Alama ya Posti,ujenzi wa chemba, uchimbaji wa Mitaro na ufukiaji wake na Kuweka Tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo 10m³ (Tanki ya Plastiki) na Kuweka Vifaa vya Kisima.

Mkataba huu wenye Namba:TR203/2025/2026/W/08 una thamani ya
TZS 575,423,966.91 umeanza rasmi tarehe 13.03.2026

Utiaji saini huo umeshuhudiwa na wajumbe wa Menejimenti wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Suwasa Ndg Sebastian V. Warioba pamoja na Mhandisi Hamis Jumanne Mkurugenzi wa Kampuni na Katibu wa Mradi Mohammed Selemani.
#kazinaututunasongambele