Wizara Ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida

SUWASA YATOA ELIMU YA MAJISAFI NA USAFI WA MAZINGIRA KWA WANANCHI WA MANISPAA YA SINGIDA.


Katika kuadhimisha wiki ya Maji kitaifa ambayo hufanyika kila mwaka, Mnamo Tarehe 18 na 19 Machi, 2026 maeneo ya Stendi ya Zamani na Soko Kuu Suwasa imetoa Elimu kwa wateja wa maji, wananchi na wadau mbalimbali wa Manispaa ya singida kuhusu masuala mbalimbali ya huduma ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira.


Mambo yaliyotolewa elimu kwa Umma ni pamoja na Mfumo mpya wa maunganisho mapya kwa njia ya mtandao, Bili za maji na ulipaji bili kwa wakati, Usajili wa kadi za ewater, Utoaji wa taarifa mbalimbali kama mivujo, wizi wa maji na Mita pamoja na uharibifu wa miundombinu ya maji kwa makusudi, Namna ya kufanya malipo ya maji, Mkataba wa huduma kwa wateja.


Akifungua tukio hilo la utoaji wa  Elimu kwa Umma Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndg Hosea Maghimbi amewaeleza wananchi, wateja na wadau mbalimbali wa Manispaa ya Singida watumie vizuri Elimu hii ili kupata ufahamu wa Huduma za Maji,  kuweza kuwasilisha malalamiko au changamoto mbalimbali zinazowakabili ili ziweze kutatuliwa.


Katika zoezi hilo lililochukua Siku  mbili malalamiko na maoni mbalimbali yamepokelewa na kufanyiwa kazi. 

##Kazinautu tunasongambele