SUWASA YATOA ELIMU JUU YA UTUNZAJI WA MIUNDOMBINU YA MAJI ENEO LA UNYAMBWA
Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira singida (SUWASA) jana tarehe 27.04.2026 imetoa Elimu juu ya utunzaji wa miundombinu ya maji katika eneo la unyambwa.
Elimu hii imetolewa kufuatia kujitokeza kwa uharibifu wa miundombinu ya mabomba wa mara kwa mara katika eneo hilo hali iliyopelekea wananchi kukosa huduma muhimu ya maji na kusababisha hasara kubwa ya fedha kwa Mamlaka.
Aidha Wataalamu kutoka Suwasa kwa kushirikiana na viongozi wa mtaa akiwemo Ndg Selemani Hassan Ikingu Mwenyekiti wa kitongoji Cha Mangua Mpyughu Unyambwa wametoa rai kwa wananchi na kuwaasa kuacha mara moja vitendo hivyo vya uharibifu wa miundombinu ya maji na kuhakikisha wanakuwa mstali wa mbele kuilinda kwani ni kwaajili ya faida yao na jamii kwa ujumla.
Pia wataalamu wa Suwasa walishauri kiundwe kikundi shirikishi kwaajili ya kuzunguka maeneo yote yenye miundombinu ya maji ili kuondoa changamoto hizo zinazojitokeza
Aidha wameeleza kuwa kwa uharibifu uliofanyika Mamlaka inaendelea na utaratibu wa Matengenezo ili kurejesha huduma ya maji safi na Salama kwa wananchi wa Unyambwa.
##Kazinautu tunasongambele