WATUMISHI WA SUWASA WASHIRIKI MAFUNZO YA SHERIA MPYA YA UNUNUZI WA UMMA YA MWAKA 2023 NA KANUNI ZAKE GN. NO. 518 YA MWAKA 2024.
Watumishi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Singida leo Tarehe 23.03.2026 wameshiriki Mafunzo ya Sheria Mpya ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2023 na kanuni zake GN NO. 518 ya mwaka 2024.
Mafunzo hayo yanaongozwa na watumishi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Ndg Lusekelo Kamwela ambaye ni Afisa Ununuzi na Msimamizi wa kanda ya kati Tabora na Ndg Tika Hamis Meneja PPRA Makao Makuu Dodoma ambapo mafunzo hayo ni ya siku 5 kuanzia Tarehe 23.03.2026 hadi 27.03.3026
Mafunzo haya yamejikita zaidi katika kujenga uelewa wa Taratibu na Sheria za Manunuzi ya Serikali ikiwemo, Historia ya Sheria za Ununuzi wa Umma kama Misingi Mikuu ya Sheria ya Umma, Taasisi mbalimbali katika usimamizi wa ununuzi wa Umma, Mpangilio wa kitaasisi Kwenye ununuzi wa umma, Njia na michakato ya ununuzi wa Umma, Uondoshwaji wa mali za umma, utaratibu wa mchakato wazabuni, usimamizi wa mikataba, usimamizi wa ugavi, Nest pamoja na utatuzi wa migogoro.
Akifungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi ndg Hosea JP.Maghimbi amewasihi watumishi kushiriki kikamilifu katika Mafunzo hayo kwani yatawajengea uwezo na kuwasaidia kuongeza uelewa na ufahamu wa masuala mbalimbali ya Sheria za Ununuzi wa Umma na Ugavi.
##kazinaututunasongambele