SUWASA YAANZA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA MAJI KWAAJILI YA UBORESHAJI HUDUMA MAJISAFI ENEO LA MTIPA MASHARIKI.
Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Singida imeanza rasmi utekelezaji wa Mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji safi katika eneo ya Mtipa Mashariki lililopo Singida Manispaa Kata ya Mtipa.
Mradi huu unahusisha ujenzi wa mnara wa tangi wenye urefu wa MITA 6 , uchimbaji wa mitaro na ulazaji wa mabomba pamoja na uwekaji wa miundombinu ya kisima na uwekaji wa tangi (plastic tank 10m3).
Mradi huu unagharimu jumla ya kiasi cha TZS 67,000,000.
Katika Mradi huu vituo vya kuchotea maji viwili yaani (viosks) vitajengwa.
##Kazinautu tunasongambele.