Wizara Ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida

SUWASA YAANZA UKARABATI WA MATENKI YA MUUNGANO NA SENENE


Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Singida(SUWASA)imeanza utekelezaji  wa Mradi wa ukarabati wa matenki ya kuhifadhia maji

Matenki ambayo yameanza kukarabatiwa ni MUUNGANO lenye ujazo wa lita 50,000 lililopo kanda ya Ikungi na tenki la Senene lenye ujazo wa lita 100,000 lililopo katika kanda ya Iguguno ambapo maeneo haya yanahudumiwa na Suwasa.

Ukarabati huo una lengo la kudhibiti uvujaji wa maji kwenye matenki hayo na  unagharimu  kiasi cha  TZS  12,992,000

##kazinaututunasongambele