WANAWAKE SUWASA WASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE MKOA WA SINGIDA
Wanawake wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) washiriki Maadhimisho ya Siku ya Wanawake ngazi ya Mkoa, yaliyofanyika katika Viwanja vya ... Wilaya ya Kiomboi, Singida yaliyofanyika tarehe 7 Machi 2026. Mgeni Rasmi katika Maadhimisho hayo alikuwa Mhe. Salma Kikwete (Mb) ambaye pia ni Mke wa Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete. Mhe. Salma amewahimiza wanawake wasibweteke kwa kuwategemea wanaume, bali wajishughulishe kutafuta maendeleo yao wenyewe, ili wasonge mbele. Ametoa wito kwa jamii kumwendeleza mtoto wa kike kwa kumpatia elimu ili aweze kupata fursa na kushika nafasi mbalimbali za uongozi. Aidha amempongea Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumtua Mama ndoo kichwani, kupitia miradi ya Maji Tanzania nzima, kwani amemsaidia mwanamke kuepuka na kutembea umbali mrefu kutafuta Maji. Aidha amempongeza kwa kujenga shule za Vipaji maalum kwaajili ya watoto wa kike Tanzania kote.Ameitaka jamii kurejea katika tamaduni zetu kwani ndio msingi wa maadili ya Taifa letu. Pamoja na hayo amepongeza Uongozi wa Mkoa na Wilaya.kwa maandalizi mazuri ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Mkoa wa Singida. Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego akieleza maendeleo ya Mkoa wa Singida katika Sekta mbalimbali, ametoa Shukrani za dhati kwa Mgeni Rasmi kwa kuitikia wito na kufika kushiriki Maadhimisho hayo pamoja na wanawake wa Mkoa wa Singida.