Wizara Ya Maji

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida

MHANDISI RAMADHANI MTINDASI
MHANDISI RAMADHANI MTINDASI
Mkurugenzi Mtendaji
KAribu SUWASA-Ninayofuraha kukukaribisha katika tovuti ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA). To...

Habari Mpya
ALIYEKUWA MKURUGENZI MTENDAJI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA AFANYA MAKABIDHIANO YA OFISI NA MKURUGENZI MPYA WA SUWASA MHA. RAMADHANI MTINDASI
ALIYEKUWA MKURUGENZI MTENDAJI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA AFANYA MAKABIDHIANO YA O ..
11-06-2026 16:09:46
Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) Bw. Sebastian V. Warioba akiwa na Mkurugenzi Mpya Mhandisi Ramadhani Mtindasi na Menejimenti ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira wamefanya kikao cha  makabidhiano ya Ofisi leo tarehe 11.06.2026 mara baada  ya kuteuliwa kituo kipya cha kazi na Mh. Waziri wa Maji Jumaa Awesso kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira Sengerema(Seuwasa)Bw. Sebastian V. Warioba pamoja na Management yote ya Suwasa wamemkaribisha Mkurugenzi Mpya Mha. Ramadhani Mtindasi katika Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) na kumsihi aendelee kufanya kazi Kwa bidii ili kufikia Malengo ya SUWASA Kwa Wateja wa Singida kwani Singida wanahitaji sana Huduma yake. Pia wamemtakia kila la Kheri katika Majukumu yake Mapya ya Kazi na kuishi vyema na Watumishi.Aidha Mkurugenzi mpya  Mh. Ramadhani Mtindasi amepokea Vema ukaribisho huo na Kumshukuru Bwa Sebastian V.Warioba Kwa kumkaribisha vema SUWASA na kumuahidi kuwa atafanya kazi Kwa bidii ili kufikia Malengo ya WanaSingida na kuhakikisha huduma ya Majisafi na usafi wa Mazingira inakuwa endelevu. Pia ameiomba  Menejimenti ya SUWASA kuwa na  ushirikiano katika Kutekeleza Majukumu yake Mapya ya Kazi kwani yeye amekuja kufanya kazi na Watu Kwa Upendo na  Kwa Ushirikiano.Nae Kaimu Mkurugenzi wa Huduma Kwa Wateja Ndg Hosea JP. Maghimbi amemshukuru Bw. Sebastian  V. Wariob...
SUWASA YASHIRIKI MAADHIMISHO YA MEI MOSI KIMKOA SINGIDA
SUWASA YASHIRIKI MAADHIMISHO YA MEI MOSI KIMKOA SINGIDA
02-05-2026 10:40:12
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) imeshiriki maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi yaani Mei Mosi Iliyofanyika kimkoa katika uwanja wa Bombadia ambapo hii ni kuimarisha  uhusiano na mshikamano thabiti baina ya  wafanyakazi wake.Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima  Dendego, amewapongeza watumishi wote wakiwemo wa SUWASA kwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi na kuhakikisha wanamsaidia Rais katika kuwatumikia wananchi hali inayochangia kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.Katika tukio hilo, Mkuu wa Mkoa alipata fursa ya kuwatunukia vyeti watumishi hodari kutoka taasisi mbalimbali, wakiwemo watumishi wa SUWASA. Watumishi hao walitambuliwa kwa juhudi zao, nidhamu na utendaji bora kazini, hatua inayolenga kuhamasisha hari ya kazi na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa jamii.Aidha, jumla ya watumishi wanne (4) kutoka SUWASA wametunukiwa vyeti vya kutambua uhodari wao katika utendaji wa kazi ambapo  Vyeti hivyo vimetolewa kama ishara ya kutumbua  na kuthamini mchango wao katika taasisi.Akizungumza wakati wa utoaji wa vyeti, Halima Dendego aliwahimiza watumishi hao pamoja na wengine kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi na uwajibikaji ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za maji.Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ilikuwa:“Kazi zenye staha ni nguzo imara kwa maendeleo endelevu katika utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050.”